Jumanne, 30 Agosti 2016

Crazy GK ageukia kwenye muziki wakuimba

Msanii wa Kundi la East Coast, King Crazy GK ameamua kuingia studio na kuandaa wimbo wa kuimba

Rapper huyo amesema kuwa ushindani uliopo kwenye game la muziki ni tofauti na zamani hali ambayo imemfanya abadilike.
“Nimeamua kuimba lakini ni kutokana na game la Tanzania kubadilika,” GK alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Zamani tulikuwa tukishindana sisi wa Tanzania kama Juma Nature, AY na wengine lakini kwa sasa muziki wa bongo ume’change’ na kuingia mpaka wakina Wizkind, so kubadilika muhimu”
GK amesema ujio wake mpya utaweza kuleta ushindani na kumuweka sehemu nzuri katika muziki wa Tanzania pamoja na kimataifa.

Ijumaa, 5 Agosti 2016

Nina filamu kubwa zaidi ya Kigodoro inakuja – Zamaradi

Zamaradi Mketema amesema yupo mbioni kuachia filamu mpya ambayo anasema itakuwa gumzo.  Akiongea na Bongo5, Zamaradi amesema filamu hiyo itakuwa tofauti na kwamba awali alipanga aiite Mchepuko lakini amebadilisha jina baada ya kuw
epo nyingine yenye jina hilo.Amesema bado ni mapema kusema itaitwaje lakini amedai kuwa ni tofauti kabisa na Kigodoro, filamu iliyompa tuzo. “Tumetoka kwenye upande wa Kigodoro kabisa tuko sehemu nyingine tofauti kabisa,” amesisitiza.

Bale, Griezmann na Ronaldo kuwania tuzo ya mchezaji bora wa UEFA


Shirikisho la Soka Barani Ulaya UEFA, limetoa rasmi majina ya wachezaji walioingia kwenye hatua ya mwisho ya kuwania tuzo ya mchezaji bora barani Ulaya mwaka huu
Wachezaji walioingia kwenye tatu bora ya mwaka huu ni Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gareth Bale (Real Madrid) na Cristiano Ronaldo (Real Madrid).
Hii ni orodha ya wachezaji waliofanikiwa kuingia kwenye kumi bora; Luis Suárez (Barcelona), Lionel Messi (Barcelona), Gianluigi Buffon (Juventus), Pepe (Real Madrid), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Manuel Neuer (Bayern München), Gareth Bale (Real Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Thomas Müller (Bayern München).
                                                             Tuzo hiyo itatolewa mjini Monaco mwezi August 25.

Alhamisi, 4 Agosti 2016

Fid Q akiri script za video alizoandika zilipata video mbovu, asema Walk it Off ilimfumbua macho (Video)

Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q, amekiri kuwa video zake nyingi ambazo aliziandika script mwenyewe zilifeli
“Kwenye Walk if Off niliamua kwenda extra miles kidogo sababu siku zote idea za video ninazo, script najua kuandika vizuri lakini kila kichupa kikitoka kinatokea ovyo,” Fid ameiambia Bongo5.
“Kwahiyo nikaona isiwe issue, labda nisikilize watu wanasemaje, nikaamua kujisachi nikaenda South na ukweli nimegundua kuwa penye nia na uwekezaji huwezi kufeli. Kwahiyo Walk it Off imekuwa video bora ya muziki Afrika Mashariki,” ameongeza.
Video hiyo ilishinda tuzo za ZIFF 2016.
Pia ngoma hiyo itatumia kama soundtrack kwenye documentary ya Uingereza na pia imefanya vizuri kwenye charts za barani Ulaya. Fid amesema mashabiki watarajie ngoma mpya siku ya birthday yake August 13 na anaweza kuachia ngoma mbili kwa mpigo.

Jumatano, 3 Agosti 2016

DJ

Dj mix - Regenteshiwakwe http://www.audiomack.com/album/regent-eshiwakwe/regenteshiwakwe

Iggy Azalea: Sina uhusiano na French Montana

Wiki iliyopita rapper Iggy Azalea na French Montana walionekana pamoja huko jijini Las Vegas, walikohudhuria show ya Jennifer Lopez, Caesar’s Palace na kisha kula bata pamoja hadi asubuhi.
Wakati ambapo wengi walihisi kuwa wawili hao walikuwa wakielekea kuwa na uhusiano wa kimapenzi, Iggy amekanusha tetesi hizo wakati akihojiwa kwenye E! News kwenye hafla ya 2016 Maxim Hot 100 mwishoni mwa wiki. “No, we’re [just] collaborating,” alisema kujibu swali la kama wako pamoja kimahusiano. “I’ve got another single coming out with French Montana, so we recorded it while I was in Las Vegas last week. It should be having a music video filmed to it in the next few weeks,” aliongeza. Mwezi uliopita Iggy alitangaza kuachana na mpenzi wake, Nick Young baada ya kuwa pamoja kwa zaidi ya miaka miwili. Alimtuhumu Nick kwa kumpa mimba mama wa mtoto wake wa kiume.

Waziri Mkuu ayakataa madawati ya msaada, ‘huu si wakati wa kupokea vitu vibovu’

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati, uliotolewa na Wakala wa Misit           Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekataa kupokea msaada wa madawati, uliotolewa na Wakala wa Misitu TFS Tanzania