Jumatano, 3 Agosti 2016

Stamina awachana wasanii wa Bongo, asema ni wanafiki na hawana upendo

Rapper Stamina amechukizwa na tabia ya wasanii wa Bongo anaowaelezea kama watu wasio na upendoushirikiano kwa wenzao                                                                                                  
Staa huyo aliyeachia remix ya wimbo ‘Mmeniroga’ akiwashirikisha Roma na Jay Moe, ameandika kwenye Instagram                                           
''Tabia ya kutopeana tafu wenyewe kwa wenyewe ndo inaleta matabaka kwenye mziki. Mwenzako ana show sehemu, au ana nyimbo yake mpya anakutumia cover ya wimbo au ya show yake unaipata kabisa ila hutaki kupost tu. Cha ajabu za wengine ambao ndo unaamini washkaji zako unazipost fresh tu kwa mbwembwe zote.
Mtu mpaka ana namba yako maana yake tayari mnajuana na mna ukaribu pia, hata kama hamna ukaribu ila sababu ni msanii mwenzie we mpe tu support. Mnasubiri mpaka mtu afariki/afe ndo mnajifanya kupost r. I. P wakati hawezi hata kuona hiyo post yako.
Mnasubiri mpaka mtu awe ameathirika na madawa, au kapigika kimaisha ndo mnajifanya kupost picha au viclip vya video na kujifanya mnahuzunika. Me nikifa kausha tu usipost maana sitoona wala haitosaidia kama kipindi niko hai hukufanya hvyo.
#UNAFKI TU#''

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni