Ijumaa, 5 Agosti 2016

Nina filamu kubwa zaidi ya Kigodoro inakuja – Zamaradi

Zamaradi Mketema amesema yupo mbioni kuachia filamu mpya ambayo anasema itakuwa gumzo.  Akiongea na Bongo5, Zamaradi amesema filamu hiyo itakuwa tofauti na kwamba awali alipanga aiite Mchepuko lakini amebadilisha jina baada ya kuw
epo nyingine yenye jina hilo.Amesema bado ni mapema kusema itaitwaje lakini amedai kuwa ni tofauti kabisa na Kigodoro, filamu iliyompa tuzo. “Tumetoka kwenye upande wa Kigodoro kabisa tuko sehemu nyingine tofauti kabisa,” amesisitiza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni