Jumatano, 3 Agosti 2016

Rama Dee atoa ujumbe huu kwa vijana wapenda maendeleo

Muimbaji huyo ambaye anafanya poa na video yake ya wimbo ‘Mazoea’, amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kutoa nukuu mbalimbali ili kuwajenga vijana katika kufanya kazi. “Unamchambua Kikwete kwa miaka yote 10 ukiwa kijiweni, leo umeanza na Magufuli tena!! Ila kumbuka wao wapo kazini pale, na wanalipwa mshahara. Kijana mwenzangu please fanya mambo yako, harakati nzuri ni kupambana kutimiza ndoto yako, mwana harakati mwenye kusema anafanya harakati huku akipokea mshara serikalini na kulinda familia yake huyo sio mwana harakati nafikiri ni mfanya Kazi Kama wafanya kazi wengine tu!!,” aliandika Rama Dee kupitia facebook. Aliongeza, “Umefikia wakati wa kila kijana kupambana ili kushinda mapambano ya kuifikia ndoto yako na malengo!! Nashukuru nimepata marafiki wazuri sana,wenye kujituma na kujielewa!. Kitu rahisi katika maisha angalia kitu ukipendacho na ukiwezacho kukifanya usifuate ndoto za watu utaishia njiani lazima,aidha utaumia!. Wewe kwanza!!! Ram
a Dee,”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni