Alhamisi, 4 Agosti 2016

Fid Q akiri script za video alizoandika zilipata video mbovu, asema Walk it Off ilimfumbua macho (Video)

Rapper Fareed Kubanda aka Fid Q, amekiri kuwa video zake nyingi ambazo aliziandika script mwenyewe zilifeli
“Kwenye Walk if Off niliamua kwenda extra miles kidogo sababu siku zote idea za video ninazo, script najua kuandika vizuri lakini kila kichupa kikitoka kinatokea ovyo,” Fid ameiambia Bongo5.
“Kwahiyo nikaona isiwe issue, labda nisikilize watu wanasemaje, nikaamua kujisachi nikaenda South na ukweli nimegundua kuwa penye nia na uwekezaji huwezi kufeli. Kwahiyo Walk it Off imekuwa video bora ya muziki Afrika Mashariki,” ameongeza.
Video hiyo ilishinda tuzo za ZIFF 2016.
Pia ngoma hiyo itatumia kama soundtrack kwenye documentary ya Uingereza na pia imefanya vizuri kwenye charts za barani Ulaya. Fid amesema mashabiki watarajie ngoma mpya siku ya birthday yake August 13 na anaweza kuachia ngoma mbili kwa mpigo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni